Viungo vya Juu
“ Kituo Cha Fursa ”
Karibu Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa
Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa kipo Mkoa wa Morogoro, Manispaa ya Morogoro Mjini, umbali wa kilomita 8 kutoka katikati ya mji katika Kata ya Bigwa.
Chuo kinatoa mafunzo ya muda mrefu hadi miaka mitatu katika ngazi za NVA I, II na III pamoja na mafunzo ya muda mfupi katika fani mbalimbali zinazolenga kuwawezesha wahitimu kujiajiri na kuajirika.
Mafunzo ya NVA Level I, II na III kwa muda wa hadi miaka mitatu.
Mapishi na Lishe, Ushonaji, TEHAMA pamoja na Tailor Made Courses.
Programu maalumu kwa wasichana waliokosa kuhitimu elimu ya sekondari katika mfumo rasmi kutokana na sababu mbalimbali.
Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 17 na kuendelea, mwenye uwezo wa kusoma na kuandika vizuri.
Chagua kozi inayokufaa na uanze safari yako ya kupata ujuzi, maarifa na fursa za kujitegemea.